Historia ya mrembo aliyejikwaa mbele za watu na kusonga mbele

Amina Idd

Tazama Video
  • About
  • Updates
  • Comments

Amina Idd ni msichana mwenye umri  wa miaka 20 anayeishi katika kijiji cha Magole kata ya Magole Dumila  Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro .Amina alisoma shule ya msingi Muungano iliyopo katika kijiji cha Magole wilaya ya Kilosa.   Baada ya kumaliza darasa la saba hakuchaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari. Alitamani sana kuendelea na masomo lakini haikuwezekana kwa vile wazazi wake hawakuwa na uwezo wa kumlipia ada kwenye shule binafsi.

Ili kukidhi mahitaji yake Amina alianza kushiriki kazi za uuzaji wa CD za tamthiliya mbalimbali kwenye kibanda cha kaka yake huku akilipwa  kiasi kidogo cha fedha. Mwaka 2013 ilinyesha mvua kubwa na kusababisha mafuriko hivyo kusababisha uharibifu wa CD na kibanda cha biashara Hii ikawa ni mwisho wa ajira ya Amina.  Ili kujikimu  kimaisha Amina alitumia fedha kidogo aliyoipata akaanza biashara ya kununua matunda na kuyauza. Amina anakumbana na chanagmoto nyingi kama vile ukosefu wa wateja wa kutosha na hivyo kufanya matunda kuoza.

Amina hakukata tamaa alijipanga upya ili aanze biashara yake binafsi. Alibahatika kujiunga na mafunzo ya msingi yahusuyo utengenezaji wa majiko sanifu yaliyotolewa na shirika la SNV kupitia asasi ya MWAYODEO katika mradi wa OYE. Mafunzo  yalimpa ujuzi wa  kutosha wa kutengeneza majiko sanifu. Amina akaanza kutengeneza majiko kidogo kidogo mpaka   sasa  Amina ameendelea kujikita kwenye biashara hii ya utengenezaji na uuzaji wa majiko sanifu ambayo yana wateja wengi kutokana na ubora wake na kuwa ni majiko rafiki kwa mazingira.

Changamoto kubwa anayokumbana nayo ni ukosefu wa upatikanaji wa malighafi za kutengenezea bidhaa hizo hasa mabati na udongo maalumu kwa kazi hiyo. Hii inatokana na kukosa mtaji wa kutosha wa kununulia mali ghafi hizo.

Ndipo Airtel Fursa tulipoona kuna haja ya kumuwezesha Amina kwa kumpatia vitendea kazi kama mashine za kisasa zitakazomuwezesha kutengeneza majiko mengi kwa njia ya kisasa. Kwa sasa biashara ya Amina itapanuka na kutengeneza ajira kwa vijana wenzake.

Top
Logo