Jasiri mwenye moyo wa chuma
Simamia unachokiamini, utafanikiwa.

Godlisten Kimaro

Tazama Video
Moshi, Kilimanjaro
Unkown
View full episode
  • About
  • Updates
  • Comments

Godlisten Kimaro ni kijana aliyezaliwa wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro. Alibahatika kuhitimu darasa la saba, kutokana na ukata wa maisha alishindwa kuendelea na elimu ya sekondari. Ugumu wa maisha unaongezeka hatimaye baba yake alimtafutia kazi ya kuchomelea vyuma. Alipata ujuzi wa kuchomelea akiwa kama mwanafunzi kwa maana alikuwa halipwi. Uwezo wake wa kujifunza haraka ulimsaidia na baadaye Shangazi yake akamuita aende Arusha, ambapo aliendelea kujifunza Zaidi. Kwa kuwa mtembea bure si sawa na mkaa bure kijana Godlisten alipata nafasi ya kazi katika kiwanda cha kuzalisha vyuma Steel Centre. Wahenga wanasema “Ndondondo si chururu” kidogo alichokipata aliweza kukihifadhi kama akiba kiwe mtaji wa kujiajiri. Alipojiajiri alikumbana na changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa umeme uliosababisha biashara yake kudorora pia anakumbana na hasara ya kupanda kwa bei ya chuma. Sasa Airtel Fursa imemfungulia ukurasa mpya wa maisha kumuwezesha kufikia malengo yake¬† kwa kumuwezesha elimu ya ujasiriamali itakayomuwezesha kukuza biashara yake pamoja na vitendea kazi (mashine ya kuchomelea,grinder na generator) kurahisisha ufanisi wa kazi yake. Hatimaye Godlisten anaishukuru sana Airtel Fursa na kuahidi kusaidia vijana wenzake kwa kuwapa Fursa, nao wasonge mbele¬† #KipandeNaWana

Top
Logo