Kufuri moja funguo nne

Mohammed

Tazama Video
Kisarawe
Unkown
View full episode
  • About
  • Updates
  • Comments

Kupoteza wazazi wote wawili katika umri mdogo kulimwacha Mohammed katika hali ngumu na majukumu mazito ya kuwalea wadogo zake saba. Kitu ambacho kimpelekea yeye na ndugu zake kutangatanga kwa ndugu kutafuta unafuu wa maisha. Kwa msaada kutoka kwa dada yake na shemaji yake Mohammed alifanikiwa kumaliza kidato cha nne na ndio ukawa mwisho wa safari yake ya elimu. Pamoja na kulipiwa karo ya shule na dada yake, lakini bado alikuwa anatangatanga kupata mahitaji ya shule kama vitabu na sare. Akiwa masomoni alifanikiwa kupata kibarua katikanshuguli za ujenzi. Baada ya kumaliza shule kidato cha nne Mohammed hakuweza kuendelea na masomo. Kwa akiba ndogo aliyojiwekea akaweze kuanzisha biashara ya chips. Baada ya kuona biashara ya chips haina kasi ya malengo yake. Akaamua kuanzisha biashara ya mafuta kwasababu ya Toyo. Lakini alitambua fika biashara anayoifanya ya kuuza mafuta ni kinyume na sheria za nchi. Ndipo alipoamua kuanzisha biashara ya kuku wa kienyeji ambao mbali na kuazimia kupata kipato lakini pia alikuwa na lengo la kuchochea lishe bora katika jamii yake. Mohammed aliendelea kuwekeza katika biashara ya ufugaji ingawa alikumbana na changamoto nyingi ambazo ni soko la kuuza kuku, mtaji mdogo, usafiri wa kufikisha kuku sokoni. Airtel fursa kama kawaaida yetu ya kuwawezesha na kuwasaidia vijana wajasiriamali tulifika kwa Mohammed na kumpatia elimu ya biashara lakini pia tulimpa vitendea kazi na kumuongezea mtaji wa kuku na bada la kuwafugia. Kwasasa maisha ya kijana huyu yamebadilika kwa kiasi kikubwa. #MipangoSioMatumizi

Top
Logo