Mpambanaji wa mtaani

Elizabeth Mbugi

Tazama Video
Msasani, Dar Es Salaam
Unkown
View full episode
  • About
  • Updates
  • Comments

Elizabeth Mbugi ni mjasiriamali anayeishi Msasani jijini Dar es salaam. Alipata misukosuko mingi katika safari yake ya elimu ambapo ilipelekea Mama yake mzazi  kufanya vibarua ili apate kumtimizia mahitaji ya shule. Lakini hakufanikiwa kumaliza shule kwasababu ya changamoto alizokumbana nazo ikiwemo ya kuuguliwa na mama yake. Elizabeth hakukata tamaa akaamua kutafuta kibarua kwa mama ntilie ilia pate kuilisha familia yake. Kutokana na ujira aliokuwa analipwa kuwa mdogo, aliamua kuanzisha biashara ya matunda ambapo alikuwa anakwenda kununua matunda sokoni, anayatayarisha na kisha kuzunguka kuyauza mitaani na kwenye maofisi. Changamoto alizokuwa anakumbana nazo katika biashara yake ilikuwa ni kukosa jokofu la kuhifadhia matunda yakibaki hivyo analazimika kuyatupa. Usafiri wa kumfikisha sokoni na kuwafikia wateja wake. Pamoja na kuwa na vyombo vichache vya kuhifadhia matunda baada ya kuandaa. Elizabeth aliendelea kuishi kwa shida na dharau alizokuwa akizipata kutoka kwa baadhi ya wateja wake. Hakika mtembea bure sio sawa na mkaa bure ndivyo ilivyotokea kwa Elizabeth, baada ya shida na mateso mengi katika kujitafutia riziki na kukabiliana na ugumu wa maisha. Airtel fursa tukamwangalia kwa jicho la huruma na kuhamua kumshika mkono mjasiriamali huyu mdogo. Ambapo tulimpatia mafunzo pamoja na vitendea kazi ambavyo ni Bajaj, Jokofu, Vyombo na Mashine ya kusaga juice.  Kupitia biashara yake sasa anapata mahitai yote.

Top
Logo