Mrembo shujaa katikati ya shamba la ngano

Diana Moshi

Tazama Video
Dar es salaam
View full episode
  • About
  • Updates
  • Comments

Diana Moshi ni binti mwenye umri wa miaka 22 aliyezaliwa katika mkoa wa Dodoma. Katika utoto wake alikulia kwa bibi na babu kwani mama yake alifariki akiwa mdogo. Alibahatika kuhitimu elimu ya sekondari hadi kidato cha nne mkoani Dodoma.

Baada ya kumaliza kidato cha nne Diana alihamia Dar es salaam kwa lengo la kujiendeleza kimasomo alijiunga na chuo cha clearing and forwarding, lakini hakuona maisha kwenye hii fani, alitamani kujifunza mambo ya hotel lakini hakuwa na uamuzi kwani alikuwa analipiwa ada na bado alikuwa anaishi kwa watu kwa hiyo ilimbidi astahimili.

Akiwa anaendelea na masomo ya clearing and forwarding aligundua kuwa jirani na anapoishi yupo mama mmoja ambaye anatengeneza na kuuza keki mtaaani. Diana alimfuata mama  huyu na kumwomba awe anaenda kujifunza kwake namna ya kutengeneza keki. Mama huyu hakusita kumfundisha. Diana aliipenda sana kazi hii kiasi kwamba aliona kuwa ingeweza kumsaidia kufikia malengo yake na kuondokana na umaskini, tatizo likabakia kuwa ni mtaji.

Ilibidi  ajinyime hela aliyokuwa anapewa ya matumizi akajiunga na vikundi vya kuweka na kukopa  lakini bado hakuweza kufikia kiwango cha kukopeshwa mtaji jambo ambalo lilimlazimu kufanya kazi mbalimbali za vibarua ikiwa ni pamoja na kufanya kazi za kufua nguo za watu majumbani na kufanya usafi. Baada ya miezi miwili alipata fedha kiasi cha shilingi laki mbili.  Alianza kununua malighafi na kutengeneza keki za aina mbalimbali na kuziweka katika mitandao ya kijamii. Baada ya muda mfupi  alianza kupata oda na kuanza rasmi biashara ya kusambaza keki kutokana na oda alizopata. 

Kwa kuwa alikuwa anakumbana na changamoto ya vitendea kazi ndipo Airtel Fursa tulipomshika mkono kwa kumuwezesha Jiko maalumu la kuokea ( oven) moja, mashine ya kuchanganyia unga moja, Makopo ya maumbo ya keki na rangi mbalimbali za kupambia, jokofu maalum la kutunzia keki kabla hazijapelekwa kwa wateja na elimu ya biashara zaidi.

Hadi sasa Diana anasambaza keki kwa wateja mbalimbali ambapo kwanza anaziweka kwenye matangazo ya mitandao ya kijamii kama Twitter, Jamii forum, Facebook na Instagram. Pia anaweka number ya simu na kuwa mteja analetewa bidhaa popote alipo

Top
Logo