Mtaji wa maskini ni nguvu zake

Prisca George Chilumba

Tazama Video
Mtwara
Unkown
View full episode
  • About
  • Updates
  • Comments

Ama kwa hakika maji hufuata mkondo, ndicho kilichotokea kwa Prisca George Chilumba ambaye ni mama wa mtoto mmoja. Prisca ambaye makazi yake ni mkoani Mtwara alijifunza kazi ya ususi wa nyweli kutoka kwa mama yake. Maisha ya Prisca yalibadilika mara baada ya kifo cha Mama yake na Baba yake kuacha kumtunza binti huyu, haya yote yalitokea wakati Prisca yupo darasa la sita. Ugumu wa maisha ndio uliomfanya kuacha shule na kujikita rasmi katika shughuli za ususi kama kibarua katika saloon za watu. Prisca kwa kipato kidogo alichokuwa akikipata akafanikiwa kufungua saloon yake ambayo alikumbana na changamoto za kukosa vitendea kazi. Airtel fursa tulimtazama kwa jicho la huruma Prisca na kumpatia elimu ya ujasiriamali pamoja na vitendea kazi vyote katika saloon yake. Maisha ya Prisca yamebadilika kwa kiasi kikubwa kwasasa anaweza kuihudumia familia yake yote na biashara yake inaendelea kukuwa siku hadi siku. #HakunaKisichowezekana

Top
Logo