Mtende uliostawi jangwani

Maryam Mrisho

Tazama Video
Kinondoni, Dar Es Salaam
View full episode
  • About
  • Updates
  • Comments

Maryam Mrisho ni mkazi wa Kinondoni Mkwajuni jijini Dar es salaam. Alipata elimu ya msingi katika shule ya Ananasifu. Baada ya kuhitimu elimu ya msingi alishindwa kuendelea na masomo kutokana na mama yake ambaye ndiye mlezi pekee kukumbwa na maradhi. Kutokana na ugumu wa maisha ilimbidi atafute kazi. Akabahatika kupata kibarua kwa mama ntilie aliyejulikana kwa jina la Mama Kibibi. Ujira aliokuwa analipwa haukuwa unamtosha lakini kwa kubana matumizi walifanikiwa kupata kiasi kidogo cha pesa ambacho alikitumia kama mtaji baada ya kutadhurumiwa na Mama Kibibi na kuamua kuacha kazi. Pamoja na kwamba alikuwa na biashara yake ya maandazi, chapati na ice cream lakini bado alikumbana na changamoto za kukosa vitendea kazi, mtaji mdogo, na kudhalilishwa kijinsi na baadhi ya wateja wanaume. Akiwa na umri wa miaka 23 Maryam anapata mtoto, jambo ambalo linamuongezea mzigo wa kulea mtoto ambaye baba yake amemtelekeza. Ukishikwa shikilia ndivyo alivyofanya Maryam, Airtel fursa tulivyobisha hodi katika biashara yake na maisha yake kiujumla. Tukiwa kama mradi wa kijamii unaolenga kuwawezesha vijana kukuza biashara zao kwa kuwapatia mafunzo na viendea kazi bora. Tulimpa Maryam elimu ya kumwezesha kuendesha biashara yake kwa tija. Vilevile tukamkabidhi vitendea kazi ambavyo ni Jokofu, Jiko la gesi, na vyombo. Ambavyo vimefanikiwa kubadilisha maisha yake na kumwezesha kuihudumia familia yake. #UkishikwaShikilia

Top
Logo