Ndoano ya kuvuta ndoto

Maryana Magombela

Tazama Video
Mwanza
Unkown
View full episode
  • About
  • Updates
  • Comments

Maryana  Magombela ni mjasiriamali anayejihusisha na uchakataji wa dagaa na samaki jijini Mwanza. Alibahatika kuhitimu kidato cha nne  kinagaubaga hatimaye ukata wa maisha ulipelekea ashindwe kuendelea na masomo ngazi ya juu.

Katika mihangaiko ya hapa na pale alipata ajira ya kufanya kazi za usafi  katika ofisi za

Fisheries Nyegezi Mwanza. Kwa kuwa ndoto zake zilikuwa bado hazijatimia, ndipo alipoweza

kujiwekea akiba ili kiweze kumsaidia baadaye.

Jijini Mwanza Samaki ni biashara kubwa sana kiuchumi. Ndipo Maryana anathubutu kujikita katika shughuli za uuzaji samaki.

Alipata changamoto ya vitendea kazi kama Jiko na Wavu hali iliyompelekea kuandaa samaki kwa kuwabanika juu ya matofali ambapo ilikuwa inamchukua siku 2 hadi 3 kuwaandaa samaki.

Kwa kuwa  Airtel Fursa jukumu letu ni kuwawezesha vijana  ndipo tulipo ona kuna haja ya kumuwezesha kufika mbali zaidi kutimiza malengo yake. Airtel Fursa tumemshika mkono Maryana kwa kumjengea banda la kisasa la kukaushia Samaki, litakalomwezesha kukausha Samaki wake katika ufanisi wa hali ya juu. Pia tumemkabidhi pikipiki (bodaboda) itakayomuwezesha kurahisisha kufikisha bidhaa zake sokoni kwa wakati. Hatukuishia hapo kwa kuwa alikuwa na changamoto ya vifungashio, tumemuwezesha mashine ya kisasa na vifuko kwa ajili ya kufungasha samaki kwa njia ya

kisasa na kuipa thamani biashara yake.

Kwa sasa kipato cha Maryana kimeongezeka na anajivunia biashara yake.

#MimiNiMwanamkeShujaa

Top
Logo