Ng’ombe wa maskini aliyezaa.

Jonathan Tarimo

Tazama Video
Arusha
Ufugaji
View full episode
  • About
  • Updates
  • Comments

Jonathan Tarimo ni kijana wa miaka 20 anayejihusisha na shughuli za ufugaji. Jonathan alipata wazo la kujihusisha na shughuli za kilimo baada ya kumaliza elimu ya msingi. Akiwa kama kijana hakutaka kuwa tegemezi kwa familia hivyo alianza kujihusisha na ufugaji. Jonathan anakumbana na changamoto ya kutokuwa na n’gombe kama mtaji wa kuanzia. Ndipo alipo kwenda kumuomba mjomba wake N’gombe kama mtaji. Kwa bahati nzuri alipatiwa ng’ombe jike kwa makubaliano angempatia Mjomba wake  ndama wa kwanza na yeye Jonathan angemchukua ndama wa pili. Mola hamtupi mja wake mwezi desemba ulikuwa wenye Baraka kwake kwani alipata taarifa amefaulu kuingia sekondari na pia  ng’ombe wake alizaa. Kisha  kumchukua yule ndama kumkabidhisha kwa mjomba wake kama walivyokubaliana. Elimu kwanza, mnamo mwezi Januari ilimpasa aende shule na kuacha mifugo chini ya uangalizi wa baba yake. Ng’ombe wake alizaa ndama na kwa bahati mbaya ng’ombe  alifariki. Ilimladhimu kurudi tena kwa mjomba wake na akapewa ng’ombe mwingine. Pamoja na changamoto hizi, alifanikiwa kumaliza kidato cha nne. Hatimaye Airtel Fursa tukamshika mkono kijana Jonathan kutanua njia zake za kutimiza ndoto zake kwa kumuwezesha kumjengea banda la kisasa pamoja, Ng’ombe wawili pamoja na madawa kwa ajili ya Ng’ombe wake. Jonathan anazalisha maziwa kwa kiasi kikubwa na kupelekea kukua kwa kipato chake hatimaye ameajiri msaidizi kumsaidia shughuli zake za ufugaji. #AsiyefanyaKaziNaAsile

Top
Logo