Panapo shida, maarifa huongezeka
Siku zote usikubali kushindwa, pigania mpaka ujue hatima yake.

Godfrey Frank

Tazama Video
Mtwara
Unkown
View full episode
  • About
  • Updates
  • Comments

Godfrey Frank ni kijana aliyezaliwa mkoani Mtwara, alihitimu elimu ya msingi katika shule ya msingi Chikongora.  Alijiunga kidato cha kwanza shule ya sekondari St. Thomas mkoani Mtwara na baadaye akajiunga na chuo cha Bandari College na hatimaye alijiunga chuo cha Dar es salaam Maritime Institute na kusoma kozi ya International Logistics and Transportation Dhana ya elimu kama ufunguo wa maisha haimuakikishii mtu kazi kwa 100%, changamoto za maisha zilizomkabili Godfrey zilimpelekea kujiajiri ili kuziba pengo la ukosefu wa ajira katika maisha yake. Ndipo alipokaa alipojikita kwenye mradi wa kutengeneza sabuni ya unga na kuuza kwa wateja. Godfrey anakumbana na changamoto ikiwa kama wateja kutoamini bidhaa yake, uhaba wa masoko pamoja na vitendea kazi. Godfrey ni mfano wa kuigwa na jamii kwa mtazamo na hulka yake, anadhihirisha kama unaweza kuwa na mwanzo mdogo lakini ukawa na ndoto kubwa. Kupitia Airtel Fursa kijana Godfrey amewezeshwa mafunzo ya ujasiriamali kukuza elimu ya biashara yake ikiwa kutunza hesabu za biashara yake, Pikipiki ya miguu mitatu (TOYO) pamoja na vifungashio vya sabuni yake. Baada ya Airtel Fursa kumuwezesha,  ameweza kuwafikia wateja kwa wakati na kupelekea kuuza sabuni yake kwa kiasi kikubwa na kukuza kipato chake kwa kuendesha maisha yake na familia yake. #ChoziLaMnyonge

Top
Logo