Shujaa aliyekiona cha mtema kuni

Hashimu Mikidadi

Tazama Video
  • About
  • Updates
  • Comments

Hashim Nuhu Mikidadi ni kijana aliyezaliwa Mkoani kigoma, Wilaya ya Kigoma Vijijini katika kijiji cha Kiziba. Alisoma shule ya msingi Kiziba hadi alipomaliza darasa la saba. Baada ya kumaliza elimu ya msingi alihamia mkoani Morogoro ambapo alianza kidato cha kwanza hadi cha nne katika shule ya Sekondari ya Ngerengere na kuhitimu mwaka 2012. Alisoma kwa taabu kubwa kutokana na hali duni ya maisha ya wazazi wake, akiwa anaendelea na elimu ya Sekondari alianza shughuli za ujasiriamali ili kukidhi mahitaji ya shule na chakula pamoja na kusaidia wazazi wake ambao ni wazee.

Baada ya kumaliza kidato cha nne kijana Hashimu hakufanikiwa kuendelea na masomo ya juu kutokana na kupata matokeo yasiyoridhisha. Hata hivyo hakukata tamaa badala yake aliendelea na shughuli ndogo ndogo za kumuingizia kipato. 

Akiwa Mkoani Morogoro alijiunga na kikundi cha kufyatua tofali. Katika umri wa miaka 17 alianza kuweka akiba iliyopatikana kutokana na kazi ya kufyatua na kuuza matofali. Alijiwekea akiba hadi kufikisha Ths. 300,000/ ambazo alizitumia katika kilimo cha Ufuta. Baada ya misimu miwili ya kilimo Hashimu alifanikiwa kupata Shilingi  800,000/= ambazo alianzisha biashara ya kuuza nyama kwenye bucha ambayo anaendelea nayo hadi sasa.

Hashimu anakumbana na changamoto kama Mtaji mdogo ambao haukidhi mahitaji ya biashara yake ukosefu wa vitendea kazi vya kisasa katika kuleta ufanisi katika biashara yake (cutting machine, freezer  na  scale(mizani ya kisasa ya kupimia nyama) pia usafiri kama wa pikipiki   kuchukua nyama machinjioni kufikisha buchani.

Airtel Fursa hatukuwa nyuma ndipo tulipojitokeza na kumuwezesha kijana Hashimu kwa kumpatia elimu ya biashara ili kupata uelewa zaidi kuhusu uboreshaji wa bidhaa na utafutaji wa masoko  pia vitendea kazi vitakavyo mwezesha kuboresha biashara yake navyo ni  freezer, cutting machine na tumeboresha frame yake kwa kuweka tiles na mlango wa alluminium.

Top
Logo