Shujaa aliye poromosha mlima
Changamoto hazinikatishi tamaa, zinanikuza kishujaa.

Innocent Aloyce

Tazama Video
Misungwi, Mwanza
Unkown
View full episode
  • About
  • Updates
  • Comments

Innocent Aloyce ni kijana aliyezaliwa mwaka 1991, wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza. Amehitimu kidato cha nne shule ya sekondari Porobomani. Baada ya kumaliza kidato cha nne hakukuwa na msaada wa kuendelea na elimu. Majukumu ya familia yalimshinikiza kuanzisha biashara kukabiliana na ugumu wa maisha. Ndipo kijana Innocent alipoanza kilimo cha nyanya. Changamoto nyingi anakumbana nazo, ikiwa mtaji aliokuwa nao ulikuwa mdogo, vitendea kazi na hata madawa na ya mazao. Wahenga wanasema Mwanzo mgumu. Ili kuweza kutimiza malengo yake kuna safari lazima aipite, kijana Innocent akabadili kibarua na kujikita katika biashara ya kuuza mawe mlimani. Alipata kidogo kitu kilichomsogeza kuboresha mradi wake wa kilimo cha nyanya kwa kununua mbolea na madawa kwa ajili ya kutunza shamba.

Innocent hajakata tamaa anaendelea kupigania kutimiza ndoto zake. Anasimulia ndoto zake ni kuja kuwa mfanyabiashara mkubwa wa mazao ya kilimo kwa kuuza bidhaa nchi nzima na hata nje ya nchi. Innocent anad hihirisha “Umoja ni Nguvu” kwa kusema akiwa na shamba kubwa anaamini atatoa ajira kwa vijana wengine ili waweze kujinasua kutoka katika maisha magumu kupitia sera ya Kilimo Kwanza. Airtel Fursa imemsogezea mafanikio kimaisha kijana Innocent kwa kumpatia mafunzo ya ujasiriamali ili aweze kukigeuza kilimo chake kiwe biashara itayomuwezesha siku zote. Mkono mtupu haulambwi Airtel Fursa imemumwezesha  pampu ya kuvuta maji shambani pamoja na jembe la kukokotwa na ng’ombe kurahisisha kilimo chake cha nyanya. Kipato chake kimeongezeka baada ya kuwezeshwa na kupelekea kuendesha Familia kwa kipato anachopata kutokana na shamba lake la Nyanya. #IpoSikuYatakwisha

Top
Logo