Shujaa asiyepigika

Beta Zabron

Tazama Video
Bunju, Dar Es Salaam
Unkown
View full episode
  • About
  • Updates
  • Comments

Beta Zabron ni mwanadada anayejishulisha na ushonaji wa nguo ambaye anaishi Bunju jijini Dar es salaam. Kabla hajawa mshonaji alihitimu shule ya msingi Boko iliyopo jijini Dar es salaam. Hali ngumu ya maisha ikamfanya akatafute kibarua cha kufanya kazi za ndani ambacho na chenyewe hakikufua dafu. Kwa msaada wa Mama yake alijunga na Dogodogo Centre, kituo kinachojishugulisha na kutoa elimu kwa watoto walio katika mazingira magumu. Hapa ndipo Beta alipotoa ujuzi wa kushona nguo. Baada ya kuhitimu mafunzo alipata mkopo wa cherehani na kuanza safari yake ya biashara. Akiwa na umri wa miaka 18,

Beta alibeba mzigo mzima wa kulea na kuihudumia familia yake. Ingawa alikuwa na uwezo wa kushona na cherehani moja lakini bado alikuwa na changamoto kama ya kukosa ofisi ya kufanyia shughuli zake na vitendea kazi vingine. Hili halikumkatisha tamaa, aliendelea kupambana na changamoto alizokumbana nazo. Mpaka siku ambayo Airtel fursa tuliingia katika maisha ya binti huyu na kumpatia mafunzo ya ujasiriamali na biashara. Lakini pia tuliona kuna haja ya kumuongezea vitendea kazi. Hapo ndipo tulipomkabidhi mashine ya cherehani na mashine ya kudarizi, sambamba na pasi ya umeme. Kwa vitendea kazi hivi ukijumlisha na mafunzo aliyoyapata vimebadilisha maisha yake. #AtafutayeHachoki.

Top
Logo