Wanawake wasiousahau ubaharia kwa kuupata unahodha

Akilimali Group

Tazama Video
  • About
  • Updates
  • Comments

Akilimali Group ni kikundi kilichopo jijini Dar es Salaam, Wilayani Temeke kata ya mtongani. Kikundi hiki kinaundwa na wanachama wapatao kumi na wawili (12). Kikundi hiki kinajishughulisha na ujasiriamali wa kutengeneza sabuni za maji na kuziuza mitaani. Kikundi hiki kilianzishwa kwa msaada wa shirika lisilo la kiserikali liitwalo Restless lililo wapa mafunzo wasichana hawa. Malengo makuu ya mafunzo yalikuwa.  Moja; Kupunguza maambukizi ya ukimwi miongoni mwa wasichana, Pili; Kupunguza mimba za utotoni na lengo la tatu lilikuwa ni kupunguza unyanyapaa wa kijinsia. Wasichana hawa walipatiwawa  mafunzo ya ujasiriamali, ndipo  kupitia mwanachama mwenzao alikuja na wazo la kuanzisha biashara  naye ni Fatuma Rashidi ambaye yeye kwenye kikundi ni Community Volunteer( Mwezeshaji rika wa kujitolea wa Kijamii).

Baada ya wazo hili walianza kuchangishana shilingi elfu moja moja kila walipokuwa wakikutana. Biashara ya kwanza waliyoanza nayo ni kuuza matunda kama maembe, machungwa na Parachichi mitaani. Biashara hii walianza na mtaji wa elfu hamsini (50,000) walizokuwa wakichangishana wanakikundi wote kumi na mbili. Baada ya muda walipata mtaji wa shilingi laki moja na ishirini (120,000) na kukaa kikao na kuamua kubadili biashara na ndipo walianza biashara ya kutengeneza sabuni na kuziuza.

Kwa mujibu wa mwanachama Fatuma anasema kwa mwezi wanapata hadi elfu themanini kama faida kwa kikundi. (Tsh 80,000/=). Haya ni mafanikio makubwa kwenye kikundi achilia mbali changamoto wanazokabiliana nazo. Changamoto zao ni kama kukosa eneo maalumu la kufanyia biashara yao, hii huwa inawalazimu kufanyia nyumbani kwa mwanachama mwenzao (Fatuma) au wakati mwingine kwenye ofisi serikali ya mtaa iliyopo maeneo yao wanayoishi, wanakabiliwa na ukosefu wa vifungashio (chupa mfano wa chupa za tomato sause)  na vitendea kazi navyo ni ndoo kubwa za maji,ndoo ndogo za maji,mabeseni,na mwiko. Pia changamoto kubwa zaidi ni ukosefu wa dawa za kuchanganya wakati wanatengeneza sabuni hizi.

   Ndipo Airtel Fursa tulipowashika mkono na kuwawezesha pikipiki ya matairi matatu ( TOYO), madawa ya kutengenezea sabuni, marashi pamoja na mavazi maalum kwa usalama wao wakati wa utengenezaji wa sabuni.

Top
Logo